UWEKEZAJI ATCL UWE KICHOCHEO CHA UKUAJI WA UCHUMI - MAJALIWA

 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Uchukuzi kusimamia vema Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) ili kuhakikisha uwekezaji mkubwa uliofanyika unaleta matokeo chanya na kuwa kichocheo cha ukuaji wa uchumi nchini.

Mheshimiwa Majaliwa amesema hayo wakati wa mapokezi ya Ndege mpya aina ya Boeing B 737-9 Max alipomwakilisha Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan leo Jumanne Machi 26, 2024 Uwanja wa Ndege wa kimataifa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.


Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa ongezeko la ndege na huduma za usafiri inasaidia kuongeza fursa za biashara kati ya Tanzania na mataifa mengine na kuongeza upatikanaji wa fedha za kigeni kisha kuongeza idadi ya watalii wanaokuja nchini.

Aidha, Mhe. Majaliwa amesema kuwa ili kuendelea kuikuza sekta ya anga nchini, Wizara ya Uchukuzi iandae mpango wa kuongeza wataalamu wazalendo katika fani zinazohusu masuala ya ndege hususan katika eneo la matengenezo na urubani.

Akisisitiza, Mheshimiwa Majaliwa amewataka watumishi wa Shirika la Ndege Tanzania kuongeza uzalendo na kuwafichua wale wote wenye nia ya kulihujumu shirika hilo pamoja na kudhibiti upotevu wa mapato kupitia tiketi na mizigo.


“Wizara pamoja na watumishi wa wizara mfanye mpango wa ubunifu kuwafichukua wanaohujumu mapato ya shirika ili lizidi kukua kimapato” amesema Mhe. Majaliwa.

Post a Comment (0)
Previous Post Next Post