MTANGAZAJI ALLOYCE NYANDA KUONGOZA MDAHALO WA KUMTATHIMINI RAIS SAMIA HASSAN KAMA ANAUPIGA MWINGI

 


Waandishi wa Habari na wadau mbalimbali wakiongozwa na Mtangazaji wa kipindi cha The Big Ajenda kinachoruka kwenye Televishen ya Star tv,Wmekutana na Kutangaza juu ya Mdahalo mkubwa utakao wakutanisha Wandishi wa Habari pamoja na wananchi kufanya Tathimini ya Miaka mitatu ya Rais dk Samia Suluhu Hassan


Kubwa zaidi itakua ni kuangalia Miradi ya kimkakati iliyokua Ndoto ya Rais wa Awamu ya tano Hayati John Pombe Magufuli,Je Rais Samia Amefanya nini?

Amesema Mdahalo huo Utafanyika tarehe 30.03.2024 katika Ukumbi wa kwa Tunza Uliopo kwenye fukweza ziwa victoria,

Nyanda amesema kuelekea katika Siku hiyo kubwa zaidi kutakua na matukio mbalimbali,Kuanzia siku ya jumatatu ya tarehe 25.03.2024 wataungana na Wamama ambao baada ya kusikia tangazo la Mdahalo huo Wakaamua kuungana kuwafikia watoto wa shule watatoa taulo kwa shule mbili zilizopo ndani ya Halmashauri mbili zilizopo Jijini mwanza 

Kwa siku ya jumatano wataungana na Bavicha,Uvccm na baadhi ya vyama katika zoezi la Upandaji miti na Uchangiaji wa Damu katika kitengo cha Damu salama katika Hospitali ya Bugando

Zaidi tumekuwekea Video hapa Chini



By Pascal Kadushi

Post a Comment (0)
Previous Post Next Post