MIKOA 11 KUNUFAIKA NA UTAFITI NA UZALISHAJI WA MBEGU NA MAZAO

 


Jumla ya Mikoa 11 inatarajia kunufaika na shughuli za utafiti pamoja na uzalishaji wa mbegu na mazao, kufuatia makabidhiano ya vitendea kazi chini ya programu ya kuendeleza kilimo na uvuvi yaani Agriculture and Fisheries Development Programme (AFDP), inayolenga kuongeza ufanisi kwa watumishi ili kuongeza tija kwenye kilimo.


Makabidhino hayo yamefanyika tarehe 12 Machi 2024, yakiratibiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe.Jenista Mhagama (Mb), katika Ofisi yake , Mkoani Dodoma. Katika makabidhiano hayo, Wizara ya Kilimo imepokea gari 1, Taasisi ya Utafiti Tanzania (TARI) imepokea magari 2 na pikipiki 4 huku Wakala wa Mbegu wa Taifa (ASA) ikipokea magari 3 na pikipiki 3.


Hafla hiyo imehudhuriwa pia na Mhe.Shaaban Ali Othman (Mb), Waziri wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar, pamoja na Mhe. Hamza Hassan Juma (Mb), Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi kama ni Wizara zinazotekeleza programu hiyo na huku Wizara hizo zikitarajiwa kunufaika na vitendea kazi katika awamu ya ijayo.

Vifaa vilivyokabidhiwa vitawasaidia watumishi wa Sekta ya Kilimo kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi katika kusimamia miradi mbalimbali ya kilimo; ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya uzalishaji wa mbegu katika mashamba ya mbegu ya Kilimi- Tabora , Msimbazi-Kilosa , pamoja na kusimamia umwagiliaji wa mbegu katika Mashamba Mama ya mbegu ya Ilonga - Kilosa na Seliani -Arusha.

Akipokea vifaa hivyo, Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. David Silinde (Mb) amesema kuwa vitendea kazi hivi vitaboresha shughuli za utafiti na uzalishaji wa mbegu za nafaka, mafuta pamoja na mbegu jamii ya mikunde, katika kuongeza thamani, kupanua masoko ya mazao na kuongeza ajira nchini.

Hii ni awamu ya kwanza ya ununuzi wa vitendea kazi chini ya programu ya AFDP vyenye thamani ya shilingi 259,787,663 ambapo jumla ya magari 11 na pikipiki 23 zikijumuisha pikipiki 3 za miguu mitatu zimegawiwa kwenye Wizara ya Kilimo, Wizara ya Mifugo na Uvuvi na katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu).

Picha za matukio mbalimbali




By Pascal Kadushi
Post a Comment (0)
Previous Post Next Post