![]() |
Wito huo umetolewa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Kamishna Benedict Wakulyamba Wilayani Biharamuro Mkoani Kagera, alipokuwa akizungumza na uongozi wa Hifadhi ya Taifa Chato, na askari wa Jeshi la Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi ya Taifa Tanzania (TANAPA) na Wakala wa Misitu Tanzania (TFS).
CP Wakulyamba licha ya kuwapongeza askari hao kwa kazi nzuri wanazofanya, amesisitiza kuwa, uongozi wa Wizara hiyo hauta mvumilia askari askari yeyote atakae kwamisha jitihada za Wizara za usimamizi bora wa Uhifadhi hususani katika kupambana na Ujangili, Uingizwaji Mifugo Hifadhini na Uchomaji moto Misitu iliyohifadhiwa kisheria.
Awali akitoa Taarifa za ya utekelezaji wa majukumu ya Hifadhi ya Burigi Chato, Mkuu wa Hifadhi Burigi Chato, Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi ACC-Ismail Omari Ismail, amesema ndani ya muda mfupi wa uongozi wake wamefaniliwa kupamba na uingizaji wa mifugo ndani ya Hifadhi kwa asilimia 225 kutoka Januari 2022 - February 2023 mifugo 13,839 hadi 6, 154 kwa Januari 2023 - Februari 2024 na kuwa zoezi hili ni lakudumu.
Aidha ACC-Ismail kwa niaba ya watumishi wengine ameahidi kufanyia kazi maagizo yote waliopewa na uongozi wa Wizara hususani kusimamia nidhani ya askari, kubuni njia mbalimbali za kuongeza mapato ya Hifadhi (kuondokana na utegemezi) na kuimarisha mahusiano mema, na viongozi wa Serikali ngazi ya Mkoa hadi Vijiji pamoja na wanchini waishio pambezoni mwa Hifadhi.
Katika hatua nyingine CP Wakulyamba amekutana na Mkuu wa Wilaya ya Biharamuro SACP Advera Bulimba na Kamati ya Ulinzi na usalama Wilayani humo na kuupongeza uongozi wa Wilaya hiyo kwa ushirikiano unaotoa katika uhifadhi wa Hifadhi ya Taifa Burigi Chato, na kuahidi kuwa Wizara ya Maliasili na Utalii chini ya Waziri Mhe. Anjella Kairuki itaendelea kushirikiana vyema na uongozi wa Wilaya hiyo.
By Pascal Kadushi


