Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Mwalimu Hassan Masala leo Tarehe 05.03.2024,Ameendelea na ziara yake ya kusikiliza kero za wananchi katika wilaya yake yenye kata 19 Baada ya Kupita Kata ya Buswelu na Kiseke na Kusimama kwa Muda kufatia Msiba wa Taifa wa Rais wa Pili wa Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania Hayati Ali Hassan Mwinyi aliyefariki tarehe 29.02.2024 Na Rais wa Awamu ya sita ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh.Samia suluhu Hassan Kutangaza Maombolezo ya siku Saba kwa Taifa.
Siku ya Jumanne ya tarehe 05 mach 2024 Ameendelea na ziara yake ya kusikiliza kero Katika Kata ya Kawekamo,Kubwa zaidi ni Afisa Afya wa kata ya Kawekamo Bwana Paul Nataniel aliye changisha Shillingi 10,000 kwa wafanya Biashara wadogowadogo Maarufu kama Mama ntilie na kuchukua pesa shillingi 100,000 na kukaa nazo ofisini kwake zaidi ya miezi miwili pasipo Kutolea Taarifa.
Wakili Kibamba Kiamoni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela,Akitolea Ufafanunzi juu ya changamoto za barabara katika Manispaa ya ilemela ambazo mwarobaini wake wameupata,amesema siku za hivi karibuni wanategemea kupata mitambo yao ya ujenzi wa barabara.