Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu ameridhishwa na huduma za Afya zinazotolewa katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa (Kinyonga) pamoja na upatikanaji wa dawa baada ya kutembelea katika wodi mbalimbali zilizopo katika hospitali hiyo ikiwemo wodi ya kina mama wajawazito.Waziri Ummy Mwalimu ametembelea katika hospitali hiyo leo Februari 28, 2024 ambapo amesema miongoni mwa huduma alizofurahishwa nazo ni pamoja na wagonjwa kuhudumiwa kwa wakati, upatikanaji wa dawa, uboreshwaji wa miundombinu ikiwemo huduma za dharura na kuimarisha ukusaji wa mapato kwa kutumia mfumo wa ‘GOTHOMIS’
Akiwa katika ziara yake Mkoani Lindi Waziri Ummy atakagua hali ya upatikanaji wa huduma za Afya katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi (Sokoine), Hospitali za Wilaya, Vituo vya Afya




