WAKAZI WA NYAMBITI MWANZA WAFURAHIA KUREJEA KWA MAJI SAFI

 

Wakazi wa maeneo ya Ustawi na Nyambiti Kata ya Buzuruga jijini Mwanza wameipongeza Serikali baada ya huduma ya kutengamaa.

Pia wamepongeza kazi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) kwa kujitoai usiku na mchana bila kuchoka ili kuhakikisha wanapata maji baada ya miundombinu inayowapelekea maji kuathiriwa na mvua eneo la Darajani A.

Pongezi hizo wametoa kwa nyakati tofauti mbele ya Timu ya MWAUWASA iliyokuwa katika doria maalum kwenye maeneo hayo ili kujiridhisha kufika kwa huduma.


Mkazi wa Nyambiti Bondeni, Lucia Joseph amesema alishuhudia mafundi wa MWAUWASA wakipambana usiku na mchana ili waweze kupata huduma.


"Tunawapongeza sana mafundi wa MWAUWASA; jitihada zao zimezaa matunda na sasa huduma imerejea, tunayo furaha kubwa kwa hili," amesema Lucia.

Naye Lunani Lumbecha Mkazi wa Nyambiti alithibitisha kurejea kwa huduma ya maji na ameipongeza MWAUWASA kwa kwa kuendelea kuwatembelea wateja wake ili kujiridhisha kila kaya yenye maunganisho ya maji imefikiwa na huduma.

Akizungumzia namna ambavyo MWAUWASA imejipanga katika maeneo inayohudumia, Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA, Bi.Neli Msuya amesema jukumu la kuhakikisha wananchi wanapata huduma linafanyika usiku na mchana bila kuchoka.

"Utaratibu wetu ni kuhakikisha tunasindikiza maji hadi kwa wateja wetu, na hii inafanyika kwa mafundi kuhakikisha wanapita nyumba kwa nyumba wakishirikiana kwa karibu na wananchi kujiridhisha kama huduma imefika," Bi. Neli amebainisha.

Maeneo ya Ustawi na Nyambiti yaliathirika kwa kukosa huduma kufuatia mvua kubwa zilizoathiri bomba kubwa la inchi 12 linalosafirisha maji kuelekea katika maeneo hayo ambalo linapita katika Mto Kenge.

Mafundi wa MWAUWASA wanaendelea na doria kwa kushirikiana kwa karibu na wananchi wa maeneo husika kuhakikisha huduma inafika kikamilifu.


By Pascal Kadushi

Post a Comment (0)
Previous Post Next Post