Hospitali ya Kamanga Sasa kuanza Kufanya Oparesheni ya Mtoto wa jicho pamoja na kutibu Presha ya Macho,Hayo yamebainishwa na Mtaalamu wa Macho katika Hospitali ya Kamanga iliyopo Mtaa wa Nyegezi Mkoa wa Mwanza
Amesema Dkt Sona Mbijima,Sasa wanatoa Huduma ya Oparesheni ya Mtoto wa jicho ambao ukikomaa unaweza kusababisha Upofu,
"Mtoto wa jicho ni ukungu unaojitokeza kwenye lenzi ya jicho ambao unaweza kutokea kwa mtoto au mtu mzima na kusababisha kupungua kwa uwezo wa kuona mbali au karibu
Visababishi na Kundi lililopo kwenye kwenye hatari ya kupata mtoto wa jicho ni Kama ifuatavyo
-Umri zaidi ya miaka 40
-Historia ya kupata ajali kwenye jicho
-Wavuta sigara
-Wanywa pombe kupindukia
-Wenye matatizo mengine ya kiafya kama kisukari
-Wanatumia muda mrefu wakiwa juani
Matibabu yake -mtoto wa jicho hutolewa kwa upasuaji"
Amewataka Wananchi wasiishi kwa mazoea kwani kwa kufanya hivyo wanaweza kupata Upofu,Amewataka wazazi na walezi kuzingatia kuwachunguza watoto wao maana kabla ya tatizo halijawa kubwa.
Amewataka pia watumiaji wa Komputa,Simu,Tablet nk kutunza afya yao ya macho ingawa amesema shida hiyo haiwezi kuleta shida hiyo ya mtoto wa jicho
Dkt Sona ameyasema hayo Feb 29 2024 katika Kipindi cha Mchakamchaka Kinachoruka Kupitia Jembe fm
Florence Peter





