FAIDA ZA KULA MLO WA ASUBUHI

 


Mlo wa asubuhi una faida nyingi na ni muhimu sana kwa afya zetu kwa ujumla. Kama huwa huna ratiba ya chakula cha asubuhi na unahitaji kutunza  afya yako ni muda wako sasa wa kuingiza mlo wa asubuhi katika idadi ya milo kwa siku.

Faida zake ni kama ifuatavyo:-


1. Hupunguza risk ya ugonjwa wa shambulio la moyo.

   - inasemekana asilimia kubwa ya watu walio na ugonjwa wa shambulio la moyo huwa hawali mlo wa asubuhi.


2. Huimarisha afya ya ubongo na iwe wa kutunza kumbukumbu

     - mlo wa asubuhi husaidia kuongeza uwezo wa ubongo kufanya kazi na ku focus.  Inasemekana asilimia kubwa ya wanafunzi wanao fanya vizuri darasani huwa wanakula  asubuhi.


3. Husaidia kupunguza msongo wa ubongo (mawazo)

   - Inasemekana asilimia kubwa ya watu walio na msongo wa ubongo (mawazo) huwa hawapati / hawali mlo wa asubuhi.

4. Husaidia kujisikia mwenye nguvu zaidi na kufanya kazi vizuri.


5. Husaidia kupunguza uzito

    - kwasababu mlo wa asubuhi husaidia ku control hamu ya kula kwa siku nzima na kupunguza kula kiasi kikubwa cha chakula kwa mlo unaofuata.

6.  Kama ukizingatia ulaji bora husaidia kuupatia mwili virutubisho mbalimbali na vitamini.

Dr Emmanuel Mjoli

Post a Comment (0)
Previous Post Next Post